Baba adaiwa kumnyonga mwanaye na kisha ajinyonga

0
70

Mtoto Deniva Derick mwenye umri wa miaka miwili ameuawa kwa kunyongwa hadi kufa na anayedaiwa kuwa baba yake mzazi, Derick Mwangama (23), ambaye naye amejinyonga na kupoteza maisha, huku chanzo kikidaiwa kuwa ni mgogoro baina ya wazazi.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limesema tukio hilo limetokea Novemba 18, 2025 katika Kijiji cha Isaka, Kata ya Nkunga,Tarafa ya Ukukwe, Wilaya ya Rungwe, Mkoa wa Mbeya.

Imeelezwa kuwa kabla ya tukio hilo, baba wa mtoto huyo alikwenda nyumbani kwa mzazi mwenzie, Violeth Edward (19) ambaye ametengana nae na kumchukua kwa nguvu mtoto akiwa na hasira na kisha kuondoka naye na kutekeleza tukio hilo.

Taarifa imeongeza kuwa baada ya baba huyo kufanya tukio hilo, alichukua uamuzi wa kujinyonga kwa kutumia kamba ya manila kwenye mti wa parachichi kando ya mwili wa mtoto wake.

Send this to a friend