Baba adaiwa kumuua mtoto wa miezi mitano kisa kulialia

0
50

Jeshi la Polisi mkoani Geita linamsaka Kabilu Mayege (20) mkazi wa Mtaa wa Kilimahewa mkoani humo kwa tuhuma za kumpiga na kusababisha kifo cha mtoto wake wa miezi mitano, Leornad Kabilu kwa kutumia mkanda na kiatu.

Akizungumza mama wa mtoto huyo, Riziki Leornad, amesema mwanaume huyo humpiga mtoto akidai atamuua kwa kuwa hapendi tabia ya mtoto kulialia, jambo lililomfanya afanye kazi zake akiwa amembeba mtoto mgongoni ili asipigwe na baba yake.

Amesimulia kuwa siku ya tukio mumewe alitoka kuangalia mpira na akataka amuandalie chakula wakati mtoto amelala. Wakati anakula, mtoto alianza kulia, na mama akabaki akitoa vyombo mezani. Ndipo mume wake alienda kitandani kumuangalia alikokuwa amelala.

Adaiwa kumuua mkewe kwa kumnyima tendo la ndoa

“Akamtoa mtoto kitandani na kumbeba kifuani huku akimnyamazisha. Akaanza kumpiga makofi ya mashavuni na mbavuni akimwambia anyamaze. Nikawa namwambia muache imetosha.

Aliendelea kumpiga na baadaye akamrusha kwenye sofa. Nikaona mtoto ameanguka amelegea. Akamfuata akaendelea kumpiga na mikanda. Nikawa namzuia huku ananipiga na kuning’ata. Alimpiga sana, ndivyo ikatokea hivyo,” ameeleza.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita, Safia Jongo, amesema tukio hilo limetokea Januari 11, mwaka huu, saa saba usiku. Baada ya mtuhumiwa kutekeleza kosa hilo, alitoroka kusikojulikana.

Send this to a friend