
Jeshi la Polisi katika Jimbo la Oyo nchini Nigeria limemkamata mwanaume aitwaye Kayode Oluwaseunfunmi kwa kosa la kumbaka na kumpa mimba binti yake mwenye umri wa miaka 14.
Afisa wa serikali ambaye amethibitisha tukio hilo katika gazeti la The Guardian, amesema baadhi ya watu walifanikiwa kumuokoa msichana huyo na kuripoti tukio hilo kwa mwandishi wa habari kisha taarifa hiyo kuripotiwa polisi.
Msichana huyo, ambaye jina lake limehifadhiwa kwa sababu za kisheria na kimaadili, ameeleza kuwa unyanyasaji huo ulianza Desemba 2024.
Akiwa na ujauzito wa miezi saba sasa, amesema tangu mama yao alivyofariki dunia miaka kumi iliyopita, baba yao ndiye aliyekuwa mlezi pekee na ndugu zake wawili.
Kutokana na ujauzito huo, msichana huyo ameshindwa kushiriki katika mitihani yake ya shule ya msingi huku akipelekwa katika kituo cha watoto yatima. Katika ombi lake, msichana huyo ameiomba mamlaka kutochukua hatua kali dhidi ya baba yake.








