Baba akojolea chakula kumkomoa mke na watoto

0
48

Stars of Poverty Rescue Foundation (SPRF) kupitia mradi wake wa AWARE 2020, limembaini baba mmoja (Jina limehifadhiwa) Mkazi wa kijiji cha Damankia Ikungi mkoani Singida ambaye anadaiwa kulewa na kukojolea unga na kitoweo kwa lengo la kuwakomoa mkewe na watoto baada kutishiwa kunyimwa chakula.

Imeelezwa kuwa mtuhumiwa amekuwa akishindwa kuihudumia familia yake, na amekuwa akifanya kitendo hicho mara kwa mara licha ya kufikishwa ngazi ya kata lakini hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa dhidi yake.

Kwa mujibu wa gazeti la Raia Mwema tukio hilo liliibuliwa hivi karibuni na Salim Hassan ambaye ni Katibu wa kamati za vijiji za kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto (MTAKUWWA) wa kijiji hicho wakati wa kikao kilichohusisha jeshi la polisi, wenyeviti wa vijiji, mahakama na madiwani kwa lengo la kushughulikia kesi za watuhumiwa wa ukatili.

Send this to a friend