Baba aliyembaka binti yake asema alijua ni mkewe

0
52

Mahakama ya Wilaya ya Mpanda imemhukumu kifungo cha miaka 30 jela Augustino Michese (59) kwa kosa la kumbaka binti yake wa kumzaa mwenye umri wa miaka 16.

Hukumu hiyo imetolewa Februari 10 na  Hakimu Mkazi Mwandamizi, Rebecca Mwalusako ambapo amesema mtuhumiwa alitenda kosa hilo tarehe tofauti kati ya Mei hadi Desemba 2022 katika Kijiji cha Isinde, Mpanda mkoani Katavi.

Hata hivyo, mshitakiwa huyo wakati akisomewa maelezo ya awali, alikiri kutenda kosa hilo huku akijitetea kuwa alikuwa amelewa hivyo alijua anayefanya nae kitendo hicho ni mke wake.

Aidha, upande wa mashitaka ulipeleka mashahidi watano akiwemo mtoto aliyefanyiwa kitendo hicho ambaye alidai baba yake alimfanyia ukatili huo mara tatu huku akimtaka kutopiga kelele na kumtisha kuwa endapo angefanya hivyo angempiga na kumfanyia kitu kibaya.

Panya Road wavamia na kujeruhi wakazi wa Bunju

Mtoto huyo ameiambia mahakama kuwa pamoja na vitisho hivyo alimweleza shangazi yake kuhusu jambo hilo, huku akidai kuwa alishindwa kuzungumza na mama yake kwani ana matatizo ya akili, hivyo alihofia kuwa asingeweza kulifanyia kazi suala hilo.

Kwa mujibu wa daktari aliyemfanyia vipimo msichana huyo, ameielezea mahakama kuwa uchunguzi umebaini kuwa mtoto huyo aliingiliwa, mbali na hilo pia ameambukizwa magonjwa ya zinaa ambapo baada ya mtuhumiwa kufanyiwa vipimo aligundulika nayo.

Send this to a friend