Baba amuua mwanae kisa kung’oa karanga

0
51

Mwanaume mmoja anayejulikana kwa jina la Sikujua Simchimba, mkazi wa Kijiji cha Chizumbi, Kata ya Ukwile wilayani Mbozi mkoani Songwe anadaiwa kumpiga na kumsababishia umauti mtoto wa kaka yake, Tofa Simchimba (5) kwa kosa la kung’oa karanga zake.

Mwenyekiti wa kijii hicho, Hosea Mbelea amesema baada ya tukio hilo mtoto huyo alifichwa ndani kwa zaidi ya siku saba, na hali yake ilipozidi kuwa mbaya alipelekwa zahanati ya Kijiji cha Tensya ambapo walipewa barua ya kumhamishia hospitali ya wilaya baada ya kugundulika anavuja damu masikioni.

Baba mzazi wa mtoto huyo, Joshua Simchimba ameeleza jinsi alivyosikitishwa na tukio alililofanya kaka yake huku akisema kwamba endapo aliona ametiwa hasara angemwambia ili amlipe.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Songwe, Janeth Magomi alikiri kutokea kwa tukio hilo na kueleza kwamba mtuhumiwa anatafutwa na polisi kujibu tuhuma hizo.

Send this to a friend