Baba atuhumiwa kumlawiti mtoto wake wa mwaka mmoja

0
49

Jeshi la Polisi mkoa wa Iringa linamshikilia Amani Martin mkazi wa kata ya Nzihi Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kwa tuhuma za kumlawiti mtoto wake wa kumzaa mwenye umri wa mwaka mmoja na kumsababishia maumivu makali.

Akizungumza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Allan Bukumbi amesema mtuhumiwa alimshika mtoto wake kwa nguvu na kumfanyia kitendo hicho wakati wakiwa shambani baada ya mama wa mtoto huyo kumwacha akiwa na baba yake na kwenda kuokota kuni.

Bibi wa miaka 78 akamatwa kwa kupora pesa benki

Kamanda Bukumbi amesema mtuhumiwa huyo amekamatwa na taratibu za kisheria zinaendelea kuchukuliwa ikiwa ni pamoja na kuchunguza kiini cha tukio hilo.

Send this to a friend