Baba Jose alimtambulisha Ester kuwa mkewe na anaitwa Erica

0
39

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limesema mwanafunzi Ester Noah aliyepotea amekutwa akiwa katika chumba cha kupanga cha mwanamke aitwaye Azurat Abdul ambaye amedai binti huyo alikabidhiwa kwake na kijana anayemfahamu kwa jina la Baba Jose aliyemtambulisha kuwa ni mkewe.

Katika taarifa ya Polisi iliyotolewa Juni 23, 2023 imesema baada ya mahojiano na mama huyo alidai kuwa kijana huyo ni mteja wake wa kumletea mkaa wa magunia gengeni kwake na wakati alipomleta nyumbani kwake binti huyo alijitambusha kwa jina la Erica.

“Alipomleta takribani wiki mbili zilizopita alimueleza kuwa huyo ni mke wake ametoka mkoani Morogoro, hivyo anamuomba ampe hifadhi wakati yeye akitafuta chumba cha kupanga, na mara atakapopata chumba atakwenda kumchukua,” imesema taarifa ya Polisi.

Mwanafunzi huyo ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha Tano katika shule ya Sekondari Panda Hill alipotea tangu Mei 18, 2023 huku akiacha ujumbe akiwaaga rafiki zake na kuomba mwalimu Jimmy aache kuwafanyia wanafunzi wengine kitendo alichomfayia yeye kwani kimesababisha maisha yake kuwa magumu.

Send this to a friend