Baba wa watoto 11 ajiunga chuo kikuu akiwa na miaka 69

0
43

Baba mmoja raia wa Ethiopia mwenye watoto 11 amekuwa maarufu kwenye mitandao ya kijamii nchini humo baada ya kujiunga na chuo kikuu akiwa na umri wa miaka 69.

Tadesse Ghichile ambaye ni mkulima, hakuweza kuendelea na elimu yake baada ya kumaliza sekondari kufuatia kifo cha wazazi wake, na baadaye kuanzisha familia.

Miaka 10 iliyopita aliamua kurejea elimu yake na kisha kufanya mtihani wa kujiunga na chuo kikuu, na sasa ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Jimma katika eneo la Magharibi ya nchi ambako anatarajia kuhitimu Shahada ya Udaktari.

Hata hivyo, Tadesse ameeleza kuwa amekuwa na uungwaji mkono mkubwa kutoka kwa wanafunzi wenzake, na kwamba anatazamia zaidi kile kitakachotokea mbeleni.

Send this to a friend