Bajaji na Bodaboda ruksa katikati ya Jiji

0
17

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Innocent Bashungwa amemuelekeza Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Amos Makalla kusimamia usitishwaji wa zuio la bodaboda na bajaji kuingia katikati ya jiji la Dar es salaam lililotolewa Aprili 20, 2022.

“Namuelekeza Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mheshimiwa Amos Makalla kusimamia usitishwaji wa zuio hilo ili kutoa nafasi ya kufanya tafakuri zaidi,” amesema Bashungwa

Waziri Bashungwa amechukua hatua hiyo kufuatia uamuzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam kupiga marufuku bodaboda na bajaji kuingia katikati ya jiji isipokuwa maeneo yaliyoainishwa.

“Bila shaka nia ni njema, ila dosari ipo kwenye handling (kushughulikia) ya jambo lenyewe. Serikali yetu ya awamu ya sita inatambua na kuthamini ajira za vijana wetu wa bodaboda na bajaji kuwa ni ajira rasmi na wanajipatia riziki na familia zao,” Waziri Bashungwa.