Bajaji zasababisha mgomo wa daladala Arusha

0
51

Huduma za usafiri wa dalala zimesimama jijini Arusha huku madereva wakishinikiza kuondolewa kwa waendesha bajaji ambao wanadaiwa kufanya safari zao kinyume na taratibu.

Wakizungumza baadhi ya madereva hao wamedai bajaji zimekuwa nyingi katika jiji hilo ambazo zimekuwa zikifanya kazi sawa sawa na daladala hivyo kutaka mfumo upangwe upya ili kudhibiti bajaji hizo.

“Wito wangu kwa serikali, warudi wapange mfumo wa bajaji, bajaji ikae kama bajaji isubirie mteja sio bajaji ifanye kazi kama daladala,” amesema Lembrice Noah, mmoja wa madereva wa daladala waliofanya mgomo.

Aidha, Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Felician Mtahengerwa ameagiza safari zote za daladala zilizokuwa zimeondolewa zirudishwe na kukamata bajaji zote zinazofanya kazi kinyume na utaratibu.

Naye, Meneja wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), Amani Mwakalebela ameziondoa bajaji zote zinazofanya safari kuanzia eneo la Oysterbay kwenda eneo la Ngusero na kutaka agizo kuanza mara moja.

Send this to a friend