Bajeti ya kununua magari ya Ikulu ya Kenya yaongezeka kutoka milioni 203 hadi bilioni 6

0
66

Bajeti ya kununua magari kwa ajili ya Ikulu ya Kenya imeongezeka kutoka TZS milioni 203 hadi TZS bilioni 6, huku pia gharama za mafuta zikiongezeka kwa TZS milioni 508 kufikia TZS bilioni 2.

Ongezeko hilo ni sehemu ya bajeti ya ziada iliyowasilisha na hazina kwenye Bunge la Kenya kwa ajili ya mapitio.

Bajeti hiyo hiyo inakifungu ambacho hakijawekwa bayana chenye maelezo ‘gharama nyingine za uendeshaji,’ ununuza wa magari pamoja na gharama za usafiri.

Gharama nyinginezo za uendeshaji zimeshuhudia ongezeko la TZS bilioni 21.4, kwenye gharama ya TZS bilioni 24.4 iliyowasilishwa mwaka jana.

Kwa ujumla, bajeti ya Ikulu imekuwa ikiongezeka kwa TZS bilioni 38 na kufikia TZS bilioni 120 ambayo inajumuisha bajeti ya matumizi ambayo hajawekwa wazi, ununuzi wa magari, mafuta na TZS bilioni 4.2 ambayo ni nyongeza ya gharama za usafiri na malazi.

Aidha, bajeti hiyo imejumuisha ziada ya TZS milioni 833 zilizoelekezwa kwenye ununuzi wa mashine pamoja na TZS milioni 407 kwa ajili ya matengenezo ya magari.

Kwa upnde wa ofisi ya Makamu wa Rais, bajeti yake imeongezeka kidogo kutoa TZS bilioni 28.7 kufikia TZS bilioni 29.1, ambapo nyongeza ya TZS milioni 643 inaelekezwa kukarabati ofisi ya Waziri Mkuu Mstaafu, Raila Odinga.

Ongezeko la bajeti ya Ikulu limetajwa kuwa kubwa zaidi kushinda wizara na idara zote za serikali.

Send this to a friend