BAKWATA imetangaza Sikukuu ya Eid Julai 10

0
59

Baraza kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limetangaza kuwa Sikukuu ya Eid El- Adh’haa itakuwa Jumapili Julai 10 mwaka huu.

Sherehe hizo kitaifa zitafanyika mkoani Dar es Salaam, na swala ya Eid itaswaliwa katika Msikiti wa Mfalme Mohamed VI BAKWATA makao makuu Kinondoni kuanzia saa moja na nusu asubuhi, na kufuatiwa na Baraza la Eid.

Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Dkt. Abubakar Zubeir Bin Ali Mbwana amewatakia Waislamu na wananchi wote maandalizi mema ya Sikukuu ya Eid El-Adh’haa.

Send this to a friend