BAKWATA yakanusha taarifa ya Polisi juu ya mtuhumiwa wa ubakaji

0
52

Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera limekanusha taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi kuwa mtuhumiwa wa ubakaji wa mtoto mwenye umri wa miaka 12 ni mwalimu wa dini ya Kiislamu.

Katika taarifa iliyotolewa na BAKWATA imeeleza kuwa mtuhumiwa huyo aliyejulikana kwa jina la Haruna Ayubu Rubai (63) si imamu, sheikh au kiongozi wa dini, bali ni muumini wa kawaida wa dini hiyo, na kutoa wito kwa Jeshi la Polisi kufuta kauli hiyo ikieleza kuwa taarifa hizo zimeleta taharuki miongoni mwa waumini.

Mwanaume aliyepotea kwa miaka 34 apatikana akiwa na familia mpya

Mbali na hayo, Baraza hilo limeeleza kushangazwa na taarifa hiyo likidai kuwa ni jambo la ajabu kwa kitendo hicho cha kikatili kuhusishwa na dini.

Taarifa ya Polisi ilieleza kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo Oktoba 19, 2024 katika kituo chake cha mazoezi ya viungo kilichopo Kata ya Miembeni, Tarafa ya Rwamishenye, Manispaa ya Bukoba, ambapo anatuhumiwa kumbaka mwanafunzi wa kidato cha kwanza ambaye pia alikuwa mwanafunzi wake wa madrasa.

Send this to a friend