Balozi aliyewafananisha Waafrika na nyani arudishwa kwao

0
38

Romania imemrudisha nyumbani balozi wake kutoka nchini Kenya, Dragos Tigau na kuomba msamaha baada kuwalinganisha Waafrika na nyani.

Balozi huyo alitoa maneno hayo wakati wa mkutano katika jengo la Umoja wa Mataifa jijini Nairobi nchini Kenya Aprili 26, mwaka huu ambapo kwa mujbu wa ripoti ya shirika la habari la AFP, Tigau alisema “kundi la Waafrika limejiunga nasi” alipomwona tumbili nje ya dirisha.

Inadaiwa waliokuwa kwenye mkutano huo walijadiliana na kuamua kuficha kitendo hicho ili kumlinda Balozi, lakini Afisa wa masuala ya kigeni wa Kenya, Kamau Macharia alifichua siri hiyo Alhamisi iliyopita kupitia ukurasa wake wa Twitter ambapo alisema “Nimechukizwa na tukio hili, majaribio yalifanywa kuficha tabia mbaya aliyoifanya Balozi.”

Spika Tulia awaonya wanaotumia mitandao kumvunjia heshima Rais

Siku ya Jumamosi, Romania ilitangaza kuwa imefahamishwa tu kuhusu tukio hilo na kwamba ilikuwa imeanza utaratibu wa kumrejesha balozi wake nyumbani.

“Tunasikitika sana kwa hali hii na tunatoa pole kwa wale wote ambao wameathirika. Tabia au maoni yoyote ya kibaguzi hayakubaliki kabisa,” imesema taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Romania.

Send this to a friend