Mwanasiasa mkongwe visiwani Zanzibar, Balozi Amina Salum Ali amesema hana mpango wa kuendelea na nia ya kugombea urais kwani Rais Samia Suluhu Hassan anatosha.
Balozi Amina ambaye alichukua fomu ya urais Zanzibar mwaka 2000 pamoja na fomu ya kuomba kugombea nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2015 kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), amesema msukumo wa kugombea urais ulikuwa ni kutaka nchi ipate Rais mwanamke baada ya kuongozwa na wanaume kwa awamu zote zilizopita.
CWT yataka Polisi kutowaingilia
“Mimi niligombea urais wa Zanzibar, akateuliwa Karume (Amani Abeid Karume). Michakato yote ilikuwa migumu,” amesema na kuongeza kuwa “sigombei tena, sasa yupo mama anafanya kazi vizuri. Tunamuunga mkono, tunasifu kazi yake inaonekana.”
Aidha, Balozi Amina amesifu uongozi wa Rais Samia Suluhu na mtangulizi wake Rais wa Awamu ya Tano, Dkt. John Magufuli kwa kuhakikisha kunakuwa na utendaji wenye tija Serikalini.
Chanzo: Habari Leo