Balozi Karume aibua mapya baada ya kuvuliwa uanachama CCM

0
44

Balozi Ali Abeid Karume ameweka wazi kuwa hatakata rufaa baada ya kuvuliwa uanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) akiamini kuwa hajafukuzwa ndani ya chama hicho.

Halmshauri Kuu Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kusini Unguja ilitangaza kumfuta uanachama Balozi Karume Julai 8 mwaka huu baada ya kumweka chini ya uangalizi kutokana na kauli zake zilizoelezwa kuwa zilikidhalilisha chama pamoja na viongozi wake.

Balozi Karume amesema katiba ya nchi inatambua ngazi ya kitaifa kama eneo kuu la uamuzi, hivyo hawezi kukubaliana na uamuzi wa mkoa kumfukuza uanachama kwakuwa hauna mamlaka hayo kisheria.

“Katiba ya Tanzania inasema kutakuwa na vyama vingi vya siasa, lakini havitajengwa kwa misingi ya kidini, kikanda, kimkoa na kikabila. Hivyo, kwa mantiki hiyo, sikubali kufukuzwa na mkoa ambao hata haujanisikiliza na siwezi kukata rufaa kuhusu uamuzi batili,” amesema.

Rais Samia afanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri, Katibu na Naibu Makatibu

Aidha, Balozi Karume amesema CCM ina utaratibu wa kufuza wanachama ambapo mtoa taarifa ni Katibu Mkuu au Katibu wa Itikadi na Uenezi, lakini jambo hilo kwake halikufanyika, hivyo hakubaliani na uamuzi huo.

Kada huyo aliitwa kuhojiwa na kamati ya maadili akikituhumu chama kuwa hakijawahi kushinda kihalali kisiwani humo na kumkosoa hadharani Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Mwinyi kuhusu sera zake za kukodisha visiwa.

Pia alipinga utaratibu wa wananchi wa Kilimani kuondolewa ili kujenga ukumbi wa kimataifa na ujenzi wa Uwanja wa Amaan akidai vinakiuka utaratibu.

Send this to a friend