Balozi Karume: Niko tayari kupokea uamuzi wowote utakaotolewa dhidi yangu 

0
34

Mtoto wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar na kada maarufu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Balozi Ali Abeid Karume amehojiwa na Kamati ya Maadili ya chama hicho na kuweka wazi kwamba yupo tayari kupokea uamuzi wowote utakaochukuliwa dhidi yake.

Hali hiyo imefuatia baada ya kauli yake ya hivi karibuni katika moja ya mijadala kwenye mitandao ya kijamii, akisema CCM kipo madarakani si kwa sababu kilishinda uchaguzi, bali kwa sababu ya uwepo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK).

Balozi Karume ameitwa kwenye kamati ya maadili baada ya Makamu Mwenyekiti wa chama hicho upande wa Zanzibar kuonya baadhi ya wanachama wa  CCM kuvunja maadili na utamaduni wa chama hicho kwa kuzusha mambo ambayo yanahatarisha uhai wa CCM.

Alipoulizwa atahamia chama gani iwapo atafukuzwa CCM, amejibu kuwa hajajiandaa kufukuzwa uanachama na kama ikitokea hawezi kuhamia chama kingine chochote cha siasa, kwa sababu moyo na mapenzi yake bado yapo ndani ya CCM.

Kuhusu taarifa zilizosambaa mtandaoni akisema kadi yake ya American Express na Viza+ ni muhimu kuliko kadi ya CCM, amesema, “Ndiyo nimesema kwa sababu kadi ya CCM mara ya mwisho nilijaribu kuitumia kwenye ATM lakini haikufanya kazi.”

Send this to a friend