Balozi wa China nchini Israel akutwa amefariki nyumbani kwake

0
39

Balozi wa China nchini Israel amekutwa amefariki nyumbani kwake mjini Tel Aviv leo Mei 17, 2020.

Du Wei (58) aliteuliwa kushika wadhifa huo Februari 2020 ambapo kabla ya uteuzi huo alikuwa Balozi wa China nchini Ukraine.

Chanzo cha kifo hicho bado hakifahamiki na polisi nchini Israel wamesema kuwa uchunguzi bado unaendelea.

Wei ameacha mke na mtoto wa kiume ambao hawakuwepo nchini Israel wakati anafariki.

Hivi karibuni alinukuliwa na vyombo vya habari akiiokosoa serikali ya Marekani kufuatia kauli ya waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo, Mike Pompeo alipokuwa ziarani nchini Israel.

Pompeo alikosoa uwekezaji wa China nchini Israel na kuongeza kuwa nchi hiyo (China) imekuwa ikificha taarifa kuhusu mlipuko wa janga la corona.

Send this to a friend