Balozi wa Marekani, Dkt. Michael Battle amesema si lazima demokrasia ya nchi moja ifanane na ya nchi nyingine kwani demokrasia inapaswa kuwa ya kipekee iliyoundwa na nchi husika.
Akizungumza katika Mkutano wa Kitaifa wa Wadau wa Demokrasia ulioandaliwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) jijini Dar es Salaam amesema Demokrasia ya Tanzania inapaswa kuzingatia mazingira ya Tanzania.
“Ni muhimu kufahamu kwamba kila demokrasia haionekani sawa, kila demokrasia haipaswi kuonekana sawa, demokrasia lazima iangalie mazingira ya nchi. Demokrasia ya Tanzania haitakuwa mfumo wa utawala wa kifalme, demokrasia ya Tanzania lazima ifanane na Tanzania yenyewe, lazima ionyeshe utamaduni wa Tanzania, lazima iwe ya Tanzania pekee, lazima iwe milki ya Watanzania, lazima iundwe na Watanzania.
Sheria tatu kurekebishwa kuelekea uchaguzi mwaka 2024 na 2025
Demokrasia ya Tanzania lazima iwe ya kwake yenyewe na hakuna taifa lingine duniani linalo haki ya kuamulia Tanzania jinsi inavyopaswa kuwa,” amesema.
Battle amesema kuwa Tanzania imekuwa ikipiga hatua kubwa hivyo Marekani itaendelea kuwa washirika wa Tanzania katika kila hatua ili kusaidia kukuza demokrasia nchini.