Balozi wa Tanzania arejeshwa nchini, Usalama wa Taifa wapata bosi mpya

0
24

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko ya nafasi za uongozi mbalimbali katika Serikali ya Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania kama ifuatayo;

Amemteua balozi Hussein Othman Kattanga kuwa Balozi wa Tanzania mjini New York nchini Marekani na Mwakilishi wa Kudumu katika Umoja wa Mataifa akichukua nafasi ya Balozi Profesa Kennedy Gaston ambaye utenguzi wake umetenguliwa.

Kabla ya uteuzi huo Balozi Kattanga alikuwa Katibu Mkuu Kiongozi.

Rais Samia amemteua Moses Mpongole Kusiluka kuwa Katibu Mkuu Kiongozi. Kabla ya uteuzi huo Kisiluka alikuwa Katibu Mkuu Ikulu.

Pia amemteua Kamishna Diwani Athumani Msuya kuwa Katibu Mkuu Ikulu. Kabla ya uteuzi huo, Kamishna Diwani alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa.

Aidha, amemteua Said Hussein Masoro kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa. Kabla ya uteuzi huo Masoro alikuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu na Mkurugenzi wa Shughuli za Ndani wa Idara ya Usalama wa Taifa.