Balozi wa Zambia nchini Tanzania atumbuliwa

0
45

Rais wa Zambia, Hakainde Hichilema amefuta kazi baadhi maofisa wa serikali pamoja na mabalozi akiwemo Balozi wa Zambia nchini Tanzania, Benson Chali.

Balozi Chali amefutwa kazi ikiwa ni miaka minne tangu alipowasilisha hati zake za utambulisho kwa aliyekuwa Rais wa Tanzania, Hayati, Dkt. John Magufuli ambapo aliwasilisha hati hizo Februari 8, 2017, Ikulu, Dar es Salaam.

Baada ya kupokea hati hizo Dkt. Magufuli alisema anatarajia ujio Balozi Chali pamoja na mambo mengine utasaidia kuharakisha mchakato wa kuimarisha utendaji kazi na ufanisi wa reli ya TAZARA na bomba la mafuta la TAZAMA kwa manufaa ya nchi hizi mbili.

Mbali na balozi huyo, mabalozi wengine wa Zambia waliotumbuliwa ni Balozi wa Ujerumani, Anthony Mukwita, Balozi wa Switzerland, martha Mwitumwa, Balozi wa Ubelgiji, Nkandu Munalula na Balozi wa Uingereza, Paula Mihova.

Aidha, watendaji wengine wa serikali ambao uteuzi wao umetenguliwa ni pamoja na makatibu wakuu (20), naibu Katibu Mkuu (1), wenyeviti wa bodi (watatu) na mabalozi (13) wanaoiwakilisha Zambia katika mataifa mbalimbali.

Rais Hichilema amesema hatua hiyo ni ya makusudi ili kuleta utamaduni wa uwajibikaji serikali.

Send this to a friend