Balozi wa Zimbabwe nchini Tanzania awekewa vikwazo na Marekani

0
38

SERIKALI ya Marekani imemuwekea vikwazo Brigedia Jenerali Mstaafu wa Jeshi la Zimbabwe kutokana na kuhusika katika vifo vya raia 6 waliokuwa wakiandamana Agosti 2018 baada ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu nchini humo.

Anselem Sanyatwe ambaye pia alikuwa Mkuu wa kitengo cha ulinzi wa Rais, aliongoza kikosi cha jeshi ambacho kilifyatua risasi na kusababisha vifo vya watu 6 miongoni mwa waandamanaji jijini Harare waliokuwa wakishinikiza kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi mkuu Agosti 1, 2018.

Amekuwa mtu wa kwanza kuwekewa vikwazo na Marekani kufuatia uchunguzi wa tukio hilo, na pia mtu kiongozi wa kwanza kuwekewa vikwazo kutokana nchini humo baada ya jeshi kumuondoa Rais Robert Mugabe Madarakani.

Brigedia Jenerali Mstaafu, Anselem Sanyatwe ambaye sasa ni Balozi wa Zimbabwe nchini Tanzania alivituhumu vyama vya upinzani kuhusika na mauaji hayo wakati alipofika mbele ya kamati iliyokuwa kizchunguza mauaji hayo ikiongozwa na Rais Mstaafu wa Afrika Kusini, Kgalema Motlanthe.

Tume hiyo ilihitimisha uchunguzi wake kuwa, matumizi ya silaha yaliyofanywa na jeshi kuwatawanya waandamanaji hayakuwa sahihi wala haikuwalazimu kufanya hivyo.

Akizungumza katika kumbukumbu ya mwaka mmoja ya vifo hivyo ambapo watu wengine 35 walibaki na majeraha mbalimbali, Balozi wa Marekani nchini Zimbabwe alisema tukio hilo liliichafua nchi hiyo kimataifa na kushindwa kurudisha ushirikiano uliotakiwa.

Marekani imesema kuwa ina hofu kuwa hakuna hata mwanajeshi mmoja aliyehusika kwenye mauaji hayo amefikishwa mahakamani.

Januari mwaka huu Rais wa taifa hilo aliwaagiza wanajeshi kudhibiti maandamano ya wananchi waliokuwa wakipinga kupanda kwa bei ya mafuta ambapo takribani watu 17 waliuawa huku kukiwa na ripoti kuwa wanajeshi waliwaba wanawake.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Zimbabwe amesema kuwa Jeshi la Polisi limeanza kupewa tena mafunzo ya kukabiliana na maandamano ili kusitisha mara moja matumizi ya jeshi.

Send this to a friend