Bandari ya Dar es Salaam yaipita Bandari ya Mombasa kwa ufanisi

0
24

Bandari za Dar es Salaam, Djibouti na Berbera zimeipita Bandari ya Mombasa katika orodha iliyotolewa hivi karibuni na Benki ya Dunia juu ya bandari zenye ufanisi zaidi ulimwenguni.

Toleo la tatu la Matokeo ya Utendaji Kazi wa Bandari za Kontena Duniani (CPPI), limeiweka bandari ya Dar es Salaam katika nafasi ya 312 mwaka 2022 kati ya bandari 348 ambazo zilitathminiwa, na Bandari ya Mombasa ikishika nafasi ya 326.

Ikilinganishwa na mwaka 2021, Bandari ya Dar es Salaam imepanda kwa viwango 49 kutoka nafasi ya 361 hadi kufikia 312 mwaka 2022.

Bandari hizo zimeorodheshwa kulingana na ufanisi wao unaopimwa na muda kati ya wakati ambapo meli inafika bandarini hadi kuondoka kutoka kwenye kituo ikiwa imekamilisha zoezi la kupukua/kupakia mizigo.

Dar es Salaam ya 85 kati ya majiji tajiri zaidi duniani

Haya yanajiri wakati Bandari ya Dar es Salaam ya Tanzania katika miaka ya hivi karibuni kuwa na ushindani mkubwa, na kuahidi kuendelea kuleta meli nyingi zinazoingia katika bahari ya Afrika Mashariki kwenye bandari yao.

Takwimu kutoka Ofisi ya Kitaifa ya Takwimu ya Kenya (KNBS) zinaonyesha kiasi cha mizigo inayohudumiwa na bandari ya Mombasa kilishuka kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka mitano mwaka wa 2022, huku wadau wakitabiri kuongezeka kwa ushindani kutoka Dar es Salaam.

Jumla ya shehena ya mizigo bandarini ilipungua hadi tani milioni 33.74 mwaka 2022 kutoka tani milioni 34.76 mwaka uliopita, kulingana na KNBS.

Send this to a friend