Bangi tani 2 zachomwa moto wilayani Arumeru, Arusha

0
33

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi imekamata na kuteketeza magunia 140 ambayo ni sawa tani 2.3 za dawa za kulevya aina ya bangi wilayani Arumeru mkoani Arusha.

Kaimu Kamishna Jenerali wa mamlaka hiyo, James Kaji amesema kuwa dawa hizo zimekamatwa katika vijiji vya Engalauni na Lenglong mkoani Arusha kufuatia msako uliofanyika kuanzia Juni 30 mwaka huu ambapo mbali na dawa hizo pia watu wawili wanashikiliwa kwa kuhusika na biashara ya dawa hizo.

“Nitoe rai hasa kwa ninyi wanahabari mjaribu kuielimisha jamii biashara hii ni haramu. Kuna baadhi ya wanasiasa na watu wengine wamekuwa wakijitahidi kuhalalisha zao hili, kweli hatuwezi,” amesisitiza Kaji.

Ramadhan Kingai ambaye ni Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Arusha amesema madhara ya dawa za kulevya ni makubwa kiafya na amewataka wananchi kuota ushirikino kwa mamlaka kuhusu wanaofanya biashara ya dawa hizo ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.

Send this to a friend