Barbara ajiuzulu Simba SC, atoa sababu mbili

0
15

Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba SC, Barbara Gonzalez leo Desemba 10, 2022 ameandika barua ya kujiuzulu wadhifa wake ndani ya klabu hiyo kuanzia Januari 2023.

Barbara amesema sababu za kujiuzulu ni kutoa nafasi kwa bodi mpya ya wakurugenzi itakayochaguliwa kwenye uchaguzi ujao kupata fursa ya kuchagua Mtendaji Mkuu na menejimenti mpya itakayoendana a dira yao, pia kujipa nafasi ya kutimiza ndoto na fursa nyingine kwingineko.

“Chini ya uongozi wangu […] klabu ilipata mafanikio makubwa ndani na nje ya uwanja, ikiwemo kutwaa mataji, kuvutia wafadhili na kuanza kuheshimika kama mojawapo ya vilabu vikubwa vya soka Afrika,” ameandika.

Aidha, amewashukuru wote waliosafiri naye katika ndoto ya kuifanya Simba SC iwe kubwa kuliko ilivyokuwa huko nyuma, huku akisema “ni uamuzi mgumu sana kuacha kazi unayoipenda na uliyoifanya kwa moyo wote lakini ni ukweli pia kwamba mambo yote mazuri huwa na mwisho.”