Barcelona yataka kumsajili tena Messi

0
40

Makamu wa Rais wa Barcelona, Rafa Yuste amethibitisha kwa mara ya kwanza nia yao ya kutaka kumsajili tena Leonel Messi kwenye klabu hiyo.

Rafa Yuste amesema Barcelona imekuwa ikiwasiliana na kambi ya Messi na kwamba mchezaji huyo anajua jinsi klabu yake hiyo ya zamani inavyomthamini, hivyo angependa arudi.

Aina 5 za magari yanayotumia mafuta mengi zaidi

“Nilihusika katika mazungumzo ya mkataba miaka miwili iliyopita na bado nakumbuka jinsi ilivyokuwa ngumu kumwacha Leo Messi kuondoka,” amesema Rafa Yuste.

Kwa sasa, PSG imependekeza mchezaji huyo kusaini mkataba mpya wa kuendelea na klabu hiyo lakini bado pendekezo hilo halijakubaliwa.

Send this to a friend