Barua ya Rais Museveni akiiomba Kenya msamaha kwa Tweets za Jenerali Kainerugaba

0
61

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni ameandika barua akiiomba Kenya na Afrika Mashariki msamaha kufuatia mwanae, Jenerali Muhoozi Kainerugaba kuandika jumbe kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter zilizohusu kuiteka Nairobi na kuiunganisha Afrika Mashariki.

“Si sahihi kwa afisa wa umma, awe raia au jeshini kuzungumzia au kuingilia kwa namna yoyote ile masuala ya ndani kwa ndugu zetu,” ameandika Museveni akieleza kuwa hayo yanaweza kufanyika kupitia njia zilizokubaliwa.

Museveni ametetea uamuzi wake wa kumpandisha cheo kuwa Jenerali baada ya jumbe hizo akisema kwamba hilo ni tukio moja tu ambalo amefanya baya, lakini amefanya mengine mengi mazuri.

Pia amewaomba radhi raia wa Uganda ambao huenda walikerwa na jumbe za jenerali huyo.

[pdf-embedder url=”https://swahilitimes.co.tz/wp-content/uploads/2022/10/Statement-2_0.pdf” title=”Statement (2)_0″]

Send this to a friend