Barua ya wazi ya Zuchu kwenda BASATA na TCRA

1
52

Mwanamuziki Zuchu kutoka WCB ameandika barua ya wazi kwenda Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) saa chache baada ya video ya wimbo alioimba na Diamond, Mtasubiri Sana, kufungiwa.

Katika maelezo yake, Zuchu ameambatanisha kazi nyingine za sanaa zilizofanyika kanisani, huku akihoji sababu za wao kufungiwa lakini kazi nyingine za sanaa kuachwa.

TCRA yaufungia wimbo wa Diamond na Zuchu

Miongoni mwa kazi alizoambatanisha ni pamoja na wimbo wa Rosa Ree – I’m Not Sorry, Banana Zoro – Zoba, Filamu ya Sister Marry na filamu ya Cross My Sin- Mercy Johnson & Steven Kanumba.

Hapa chini ni barua ya Zuchu;

Ni matumanini yangu mpaka sasa kila mtu anafahamu kua Video Ya wimbo wetu pendwa “MTASUBIRI “ imesitishwa kuonekana kwenye vyombo vya habari nchini kwetu.

Nimeona bora nianze moja kwa moja kwenye mada husika. Jana Nilipokea taarifa hizi kupitia mitandao kama nyinyi tu mashabiki zetu kwamba wimbo wetu unapigwa marufuku sababu tajwa kua inaleta ukakasi kwenye jamii husika mwisho wa kununukuu .

Zuchu afunguka kuhusu uhusiano wake na Diamond na kufungiwa kwa Cheche

Awali ya yote niseme kama msanii nilietumia ubunifu kukaa chini na muongozaji wa video yetu takribani siku 4 kuunda stori ambayo kwa utashi wangu na heshima niliyonayo kwa dini zote na madhehebu yake sikuona huu ukakasi unaoongelewa hapa.

Nafahamu si kila kazi ya kisanaa itamfurahisha kila mtu lakini kuvunjia heshima dini si kitu ambacho kipo ndani ya weledi wa kazi yetu sababu tunafahamu fika tunao mashabiki wa dini zote na kulinda hisia zao ni moja ya nguzo kuu kwenye muziki hatueki matabaka.

Ifahamike kwamba mimi ndie nilishoot hiyo scene ikinataka kuwepo kanisani nikiwa nafanya mazoezi ya kwaya sio misa ni mazoezi ya kikwaya nikiwa nimevalia joho lenye stara.

Kanisa hili lipo Kisarawe na kabla ya kushoot masister walitukagua na kusikiliza kwa makini stori yetu na kuridhishwa nayo ndipo hapo tukapewa ruhusa ya kushoot.

Naomba nielekeze malalamiko yangu kwa mamlaka husika BASATA walezi na wazazi nimeambatanisha video na movie baadhi ambazo zimetoka kabla ya mtasubiri vipi hizi hazina ukakasi.

Lakini ni jamii ipi hiyo iliyoleta malalamiko mpaka nyie kufungia video iliyogharimu muda wa siku nne na pesa nyingi kuishoot tena mkaifungia bila hata kutaka kusikiliza utetezi.

Mtasubiri video ni ya kawaida sana A very innocent sweet story. Naumia sababu hii inaenda kudumaza sio tu mziki ila Tasnia nzima kwa ujumla. HAYATI Baba wa Taifa alisema “Utii ukizidi huzaa uoga ,Uoga huzaa unafiki na kujipendekeza mwisho wake Umauti.“

Huu ndio umauti wa Tasnia hii unapoanzia.

Huu ndio umauti wa Tasnia hii unapoanzia, sijui nileleze vipi hisia zangu zipokelewe kwa heshima ya kutosha na utii bila ya kuchukuliwa kama mjeuri ila kwa hili mmetuonea.

Sisi ni vijana tunaotafuta rizki bila ya kuchoka lakini pengine Wazazi wetu BASATA mmekuwa mstari wa mbele kutuvunja nguvu mbele ya jamii bila kujali hisia muda vipaji na uwekezaji unaofanyika. Hapo awali mlitoa mirabaha, wasanii wa WCB hatukunusa Top List wakati kitwakwimu za namba mauzo na ufanyaji vizuri Katika Chati zote Kasoro yenu nyinyi BASATA, COSOTA, nini shida wazazi wetu .Inawezekana vipi? Kisha hapo Tunalaumiwa kwa kutoshiriki Tuzo.

Ni wazi kuwa hii imekuwa wazi sasa kama mamlaka ya kisanaa inafanya kazi kupinga juhudi za WCB lakini pengine hii hasira mnayoipandikiza juu yetu tunaihitaji kwa mafanikio chanya yetu na mashabiki zetu wanaotupigania. Mwisho niseme kazi iendelee mashabiki zetu, maboss zetu mtusamahe sana kwa kero mnayokutana nayo haiko mikononi mwetu Wenye mamlaka washasema sisi ni nani? Tuwe na subra na msituache mana nyinyi ndo kimbilio letu la mwisho nawapenda sana, Sikukuu njema KAZI IENDELEE

Send this to a friend