BASATA: Msanii hawezi kujitoa kwenye tuzo

0
65

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limesema haiwezekani kwa msanii yeyote aliyechaguliwa kuwania Tuzo za Muziki Tanzania (TMA 2022) kuondolewa kwenye mfumo, hivyo wanamuziki waendelee kujitangaza ili waweze kupigiwa kura.

Kupitia taarifa yake imesema kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wadau wa sanaa hususani baadhi ya wanamuziki waliotangazwa kuwania tuzo hizo wakihoji namna walivyoshiriki huku wengine wakiomba kuondolewa kwenye orodha hiyo.

Filamu 6 bora za kuangalia wikiendi hii

BASATA imefafanua kuwa mchakato wa usajili wa kuwania tuzo hizo ulifanyika kwa siri kupitia mfumo wa tanzaniamusicawards.info ambapo mwanamuzi amejisajili na kupakia taarifa zake ikiwemo nyimbo na vipengele ambavyo kwa mtazamo wake amejiridhisha kuwa vinaweza kuwa na ushawishi kumwezesha kupata tuzo anayowania.

Baraza limeongeza kuwa, “BASATA inawasisitiza wadau wa Sanaa kuwa haihusiki kuingiza taarifa wala kumchagulia msanii kipengele cha kuwania katika Tuzo za Muziki Tanzania, na kwa sasa msanii haiwezekani kuondolewa kwenye mfumo.”

Send this to a friend