BASATA: Nay wa Mitego ni mtoto wetu, hatujamfungia

0
16

Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), Dkt. Kedmon Mapana, ameeleza kwamba BASATA haikumfungia mwanamuziki Emmanuel Elibariki, maarufu kama ‘Nay wa Mitego,’ kufanya maonyesho, lakini walimuita kuzungumza naye ili kurekebisha baadhi ya mambo.

Akizungumza na waandishi wa habari, alisema kwamba BASATA imempa Nay wa Mitego siku saba ili kufanya mkutano naye na kumsikiliza kuhusu wimbo wake wa ‘Amkeni.’ Pia, alisisitiza kwamba msanii huyo anaweza kuendelea na shughuli zake za muziki kama kawaida.

“Leo namwambia kwamba sisi hatujakufungia, tunakusikiliza, wewe ni mtoto wetu, tupo hapa kukulea. Kwa hiyo, tumempa siku saba tumsikilize,” alisema Katibu Mtendaji.

Orodha ya wachezaji bora wa ligi kuu ya Tanzania mwaka 2013-2023

Mnamo tarehe 9 Septemba mwaka huu, Nay wa Mitego alialikwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Central Dar es Salaam kwa mahojiano kuhusiana na tuhuma za uchochezi kupitia wimbo wake wa ‘Amkeni.’ Alikuwa kizuizini kwa takribani saa tatu. Hata hivyo, BASATA ilisema hawahusiki na kuitwa kwake polisi, ingawa walimuita mara kadhaa afike katika ofisi zao bila kuitikia wito huo.

Send this to a friend