BASATA yalaani tukio la Zuchu kutupiwa vitu jukwaani

0
102

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limelaani tukio lililovuruga utumbuizaji kwa mwanamuziki Zuhura Othman Soud (Zuchu) baada ya kutupiwa vitu jukwaani na mashabiki.

Aidha, BASATA imetoa rai kwa wadau wa Sanaa na wasanii kuheshimu misingi ya kiungwana ili kuepusha migongano isiyo na tija.

Mbali na hayo, imewataka waandaaji wa matukio kuzingatia uwepo wa mazingira salama kwa wasanii na wadau wake pindi wanapokuwa katika majukumu yao ya kisanaa.

Zuchu alikumbana na kadhia hiyo katika tamasha la Wasafi Festival Septemba 28, mwaka huu mkoani Mbeya.