BASATA yampa Harmonize siku mbili

0
43

Baraza la Sanaa la Taifa limetoa siku mbili sakata la msanii wa Bongo Fleva Rajab Abdul ‘Harmonize’ na wasanii wake Ally Omar ‘Killy’ na Rashid Mganga ‘Cheed’ kuweka sawa yote waliyokubaliana katika mkataba endapo upande mmoja utasitisha mkataba kama walivyoandikishiana.

Hayo yamebainishwa hapo na Ofisa Sanaa Mwandamizi wa Basata, Abel Ndaga katika kikao cha pili kilichopangwa kukutanisha pande zote mbili baada ya kikao cha kwanza kilichopangwa Oktoba 12, 2022 ambapo vikao vyote msanii Harmonize hakuweza kuhudhuria.

Rayvanny: Nimekua kimuziki tangu niondoke WCB

“Tumejadiliana vizuri kwenye kikao na kila kitu kimeenda sawa, tumewapa siku mbili waweke mambo sawa na kurudi hapa kwakuwa kila kitu kwenye mkataba kinajieleza,” amesema.

Hata hivyo BASATA imesema katika kikao kinachofuata lazima Harmonize mwenyewe awepo na hawatohitaji kumuona mwakilishi kwa kuwa uamuzi unakwenda kutolewa rasmi.

Wasanii hao waliokuwa chini ya lebo ya Konde Music Worldwide inayomilikiwa na Harmonize, walifikisha malalamiko yao BASATA ya kutofuatwa kwa utaratibu wa kuvunjwa kwa mkataba [uliovunjwa Oktoba 10, 2022] ikiwemo kutopewa barua rasmi.

Send this to a friend