BASATA yapiga marufuku MCs na DJs wasio na vibali

0
25

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limesema kuanzia Februari 06, 2026 waongoza sherehe, burudani na matukio (MCs) pamoja na Manju Muziki (DJs) wote wasio na vibali halali vya BASATA hawataruhusiwa kujishughulisha na kazi hizo hapa nchini.

BASATA imesema yeyote atakayekiuka agizo hilo atatozwa faini isiyopungua TZS milioni 1 au isiyozidi TZS milioni 3 au kufungiwa kujishughulisha na kazi za Sanaa kwa kipindi kisichopungua miezi sita au kufungiwa maisha.

Aidha, BASATA imesema itatoa orodha ya waongoza sherehe, burudani na matukio (MCs) pamoja na Manju Muziki ambao wana vibali halali vinavyowaruhusu kufanya kazi za sanaa.

Send this to a friend