BASATA yatangaza kuwataja wasanii ambao hawana vibali baada ya siku saba

0
42

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limetoa siku saba kwa wasanii kufanya usajili na kuhuisha vibali vyao huku likieleza kuwa watakokwenda kinyume na hapo majina yao yatawekwa hadharani.

Akizungumza Katibu Mtendaji wa BASATA, Dkt. Kedmon Mapana ametoa rai kwa wasanii zaidi ya 1000 wanaofanya shughuli za sanaa kinyume na taratibu za baraza hilo kufuata sheria ili kufanya kazi za sanaa rasmi.

“Tunatoa siku saba, leo Jumatatu halafu tunawapa tena mpaka Jumatatu, sasa wiki ijayo Jumanne tutaitana tena hapa ili kuja kutoa sasa kwamba kama bado kuna wasanii ambao watakuwa bado wanaendelea kufanya kazi bila kuhuisha vibali vyao, tutatoa orodha,” ameeleza.

Dkt. Mapana ameeleza wasanii hao wanajumuisha wanamuziki wa bongo fleva, singeli, injili, taarab, regae, dansi, hip hop, Ma Dj, Mapromota, Watozi (producers), ‘Dancers’, ‘video vixen’, wazalishaji video za muziki, mameneja, washerehesaji (Mc’s) na taasisi zinazofanya shughuli za sanaa huku akiweka wazi nia ya Baraza na serikali ni kuwezesha zaidi kwenye sekta ya sanaa.

Send this to a friend