BASATA yaufungia wimbo wa Nitasema wa Nay wa Mitego

0
28

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limeufungia wimbo wa ‘Nitasema’ wa msanii Emmanuel Elibariki maarufu Nay wa Mitego ikisema wimbo huo umekiuka kanuni ya baraza hilo.

Kwa mujibu wa taarifa ya BASATA iliyowekwa kwenye mtandao wa kijamii wa Nay wa Mitego imesema maneno yaliyotumika kwenye wimbo huo ambayo yanaishtumu Jeshi la Polisi kwa utekaji, hayana ushahidi wa kuthibitsha hilo.

Aidha, BASATA imetoa angalizo kwa vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kutopiga wimbo huo au kufanyiwa matangazo (promotion) kutokana na kuwepo kwa maneno yenye ukakasi.

Nay wa Mitego aliitwa na Baraza hilo Septemba 27, mwaka huu ili kujadili wimbo huo, ambapo mwanasheria wake alieleza kuwa baraza limemfungulia mashtaka manne yakiwemo kuvunja sheria za usimamizi wa maudhui ya sanaa na uchochezi.

Send this to a friend