Bashe aagiza Dkt. Mshindo Msola akamatwe

0
22

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe ameagiza kukamatwa na kuhojiwa Meneja Masoko wa Kampuni ya mbolea ya Minjingu, Dkt. . Mshindo Msola, msimamizi wa ghala la mbolea ya Minjingu mkoa wa Njombe na Meneja wa Kanda wa Nyanda za Juu Kusini wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Michael Sanga.

Viongozi hao wanatuhumiwa kukutwa na mifuko 776 ya mchanga katika ghala la kampuni ya mbolea ya Minjingu ambayo inadhaniwa huenda inatumika kuchakachua mbolea inayouzwa na kampuni hiyo.

Waziri Bashe ametoa maagizo hayo baada ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa wa Njombe kwa kushirikiana na kamati ya siasa ya mkoa huo kufika katika ghala hilo na kukuta shehena ya mifuko ya mchanga katikati ya mifuko ya mbolea ya Minjingu.

Bashe amesema tukio hilo ni hujuma ambayo haivumiliki, hivyo atahakikisha waliohusika wanachukuliwa hatua za kisheria.

Send this to a friend