Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema bei ya mchele imepanda kutokana na uhitaji mkubwa kutoka nje ya nchi na kuwasihi Watanzania kuongeza uzalishaji ili kuendana na masoko ya nje na kuweza kujihudumia.
Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Singida, Waziri Bashe amesema bei ya mchele kati ya mwaka 2021 na mwaka huu imepanda kwa asilimia 20.
Ameongeza kuwa Serikali inafanya mkakati wa kupeleka chakula katika maeneo ambayo bei ya mazao imepanda ili kuuza kwa bei ya chini na kupunguza gharama.
Aidha, amesema Serikali haitafunga mipaka kudhibiti usafirishaji wa mazao nje ya nchi huku akiwahimiza wakulima kuhifadhi chakula cha ziada kwaajili ya familia zao baada ya mavuno.