Bashungwa aanzia alipoishia Nape kuhusu maafisa habari wa serikali

0
58

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Innocent Bashungwa ametoa siku saba kwa mikoa 15 kutoa taarifa ya uhuishaji wa tovuti za sekretarieti za mikoa na mamlaka za serikali za mitaa.

Agizo hilo limetolewa leo Julai 2 wakati akifungua kikao kazi cha maafisa habari wa mikoa, halmashauri na taasisi zilizopo chini ya Ofisi  ya Rais – TAMISEMI.

Agizo hilo limetolewa ikiwa ni wiki chache baada Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye kutoa siku 14 kwa maafisa habari, mawasiliano na uhusiano wa Serikali (Mei 09 mwaka huu) jijini Tanga, kuhusu kuhuisha  taarifa za serikali kwenye tovuti za serikali na mitandao ya kijamii ili wananchi waweze kupata taarifa na kujua kinachoendelea kuhusu Serikali yao.

“Natoa siku 14 kuanzia Mei 14 mwezi huu kila tovuti ya Serikali  na mitandao ya kijamii iwe  na taarifa za Serikali zinazoendana na wakati kuhusu utekelezaji wa Sera au miradi mbalimbali ya Serikali, Afisa atakayeshindwa kutekeleza hili tutaachana nae,” Waziri Nape.

Send this to a friend