Bashungwa awaonya watumishi wanaojihusisha na siasa

0
75

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Innocent Bashungwa ametoa onyo kali kwa wataalamu na watumishi walio chini ya Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa wanaoingilia na kujihusisha na masuala ya siasa katika wilaya ya Temeke mkoani Dar es Salaam.

Ameyasema hayo Julai 08, mwaka huu alipokuwa akizungumza na kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Temeke na kukemea hali hiyo inayoendelea katika baadhi ya wilaya nchini, na kueleza kuwa jambo hilo linafuatiliwa kwa ukaribu na wahusika watachukuliwa hatua za kinidhamu.

Kampuni ya Bakhresa yaanza uzalishaji wa sukari

“Tunahitaji utulivu na kujenga umoja na mshikamano wa viongozi katika Wilaya ya Temeke ili utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi uweze kufanyika kwa ufanisi na weledi mkubwa, lakini kuna baadhi ya wataalam wachache wanaingilia masuala ya siasa, jambo hili nalikemea,” amesema.

Aidha, amewataka watumishi na wataalamu kujikita katika majukumu yao na kuacha masuala ya siasa yafanywe na wanasiasa kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi zinavyoelekeza.

Send this to a friend