Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Innocent Bashungwa amesema hakutokuwa na ubadilishaji wa machaguo ya shule kwa wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano.
Bashungwa amechapisha ujumbe huo katika mtandao wake wa Instagram na kusema, wanafunzi wote waliochaguliwa waripoti katika muda sahihi uliopangwa na Serikali.
“Wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano mwaka 2022, wanatakiwa kuripoti katika shule walizopangiwa kuanzia Juni 13. Hakutakuwa na kubadilisha machaguo ya shule,” ameandika.
Mei 12 Ofisi ya TAMISEMI kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu ilitangaza wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo, muhula wa kwanza ukianza June 13 huku mwisho wa kuripoti shule ikitangazwa kuwa Juni 30 mwaka huu.