Bashungwa: Serikali itawashughulikia watumishi wanaodhani zama za upigaji zimerudi

0
13

Waziri wa TAMISEMI, Innocent Bashungwa amesema Serikali haitowafumbia macho watumishi wote wa Serikali wanaodhani kwamba zama za upigaji wa fedha za Serikali zimerudi.

Akizungumza katika mahojiano na kipindi cha Clouds 36, Bashungwa amewaomba Watumishi walioaminiwa na Rais Samia Suluhu Hassan, kutekeleza wajibu wao kwa kila mmoja kwa maendeleo ya nchi.

“Dhamira ya Rais wetu siyo kushughulika na watu pasipo sababu, dhamira ya Rais anataka mambo yaende. Ndiyo maana nikasema message yake kwamba mimi kama nakosa usingizi wewe unautoa wapi. Sasa kama wewe ni mteule wake hapo lazima ufanye tafakuli kubwa sana,” amesema.

Aidha Bashungwa amesema katika TZS bilioni 149.5 zilizotolewa, wananchi wanakwenda kupata unafuu wa matibabu katika vituo vyao vya afya zitakazotumika pia kununua vifaa tiba vya kisasa katika hospitali zote nchini.

Waziri Bashungwa pia amegusia ujenzi wa soko la kisasa la Kariakoo ambao Rais Samia Suluhu Hassan ametaka soko hilo kuwa la viwango na litakalokuwa msaada mkubwa kwa wananchi.

Send this to a friend