Bashungwa: Taharuki iliyotengenezwa ya vivuko Kigamboni ni kwa maslahi binafsi

0
26

Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amewatoa hofu wakazi wa Dar es salaam wanaotumia usafiri wa vivuko eneo la Kigamboni -Magogoni juu ya taharuki kuhusu huduma isiyoridhisha inayotolewa na Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) nakueleza kuwa taharuki hiyo imetengenezwa na watu wenye maslahi binafsi.

Akizungumza katika mahojiano na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) amesema serikali imejipanga kuhakikisha inaimarisha huduma ya usafiri wa vivuko nchini ambapo tayari ameikutanisha TEMESA na Kampuni ya AZAM Marine kujadili namna bora yakushirikiana kwa pamoja kuboresha utoaji huduma ya usafiri wa vivuko katika eneo la Magogoni – Kigamboni.

“Niwatoe wasiwasi wananchi wa Dar es salaam pamoja na Kigamboni, taharuki ambayo imetengenezwa hakukuwa na sababu ya kutengenezwa. Lakini sisi tunaofahamu yapo maslahi binafsi nyuma ya utengenezaji wa hii taharuki,” amesema Bashungwa.

Aidha amesema kuanzia mwezi Agosti mwaka huu, Serikali itaanza kutekeleza mpango huo utakaotoa wigo kwa wananchi kuchagua huduma wanayotaka kutumia ya vivuko kati ya TEMESA au AZAM Marine.

Send this to a friend