Bei ya mafuta Kenya yazidi kupanda

0
74

Bei ya mafuta nchini Kenya inaendelea kuongezeka, hii ni kulingana na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Petroli (EPRA) ambayo imefanya marekebisho ya bei za mafuta ambazo zitaanza kutumika Septemba 15.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka EPRA, bei mpya za mafuta jijini Nairobi zitakuwa kama ifuatavyo: Petroli itauzwa kwa TZS 3,609.96 kwa lita, dizeli kwa TZS 3,428.3 na mafuta ya taa kwa TZS 3,455.93.

Kulingana na EPRA, bei mpya za petroli zimeongezeka kwa TZS 289.29 kwa lita, dizeli imeongezeka kwa TZS 363.66 kwa lita, na mafuta ya taa yameongezeka kwa TZS 565.1 kwa lita, ikilinganishwa na bei za awali.

EPRA pia imebainisha kuwa bei hizi zinajumuisha Kodi ya Ongezeko la Thamani ya asilimia 16 (VAT) kulingana na kifungu cha Sheria ya Fedha ya 2023.

Send this to a friend