Bei ya mafuta ya kupikia yaanza kushuka

0
50

Bei ya mafuta ya kula katika baadhi ya maeneo nchini inadaiwa kushuka baada ya bei bidhaa hiyo kuripotiwa kupanda takribani miezi kadhaa, huku lita moja ikifikia shilingi 8,000 hadi shilingi 9,000 kutoka shilingi 5,500 bei ya awali.

Kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi mmoja wa wafanyabiashara kutoka Kinondoni jijini Dar es Salaam amesema siku kadhaa zilizopita alikuwa akinunua dumu la lita 20 kwa shilingi 115,000 hadi shilingi 120,000, na sasa ananunua kwa shilingi 92,000 hadi shilingi 94,000.

Akizungumza Baby Omar mkazi wa Buguruni, Dar es Salaam amesema ndoo ndogo ilikuwa ikiuzwa shilingi 68,000 mpaka shilingi 70,000 sasa inauzwa hadi shilingi 65,000.

“Hali inaanza kurejea, kwani bidhaa hii ilipanda sana hadi wengine tuliacha kuuza kwa sababu wateja walikuwa hawatuelewi,” amesema Baby.

Watanzania milioni 2  watakiwa kurudia chanjo ya UVIKO19

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe amesema bei hizo zinashuka kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo jitihada za Serikali kuhamasisha hata wenye viwanda vidogo kuongeza uzalishaji.

Ameongeza kuwa katika bajeti hii, Serikali imepunguza hadi asilimia sifuri kodi ya mafuta ghafi ya kupikia kutoka nje, ili kuwawezesha kuyachakata na kuyauza kwa bei nafuu.

Chanzo: Mwananchi.

Send this to a friend