Bei ya Pamba kwa kilo yaongezeka kwa asilimia 92

0
40

Serikali imetangaza TZS1,560 kwa kilo moja kuwa bei elekezi ya pamba kwa msimu wa ununuzi wa mwaka 2022/2023 kutoka TZS 810 kwa kilo kwa msimu wa mwaka 2021/22, sawa na ongezeko la asilimia 92.6.

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Johari Samizi akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema kuna uwezakano wa bei hiyo kuendelea kupanda kulingana na hali ya soko kama ilivyokuwa msimu uliopita ambapo bei ya pamba ilipanda kutoka TZS 810 kwa kilo hadi 1,800 kwa kilo.

NCCR Mageuzi yamsimamisha Mbatia

Aidha, Johari ameiagiza Bodi ya Pamba nchini (TCB) kushirikiana na wadau wengine kusimamia ubora wa pamba katika soko la Kimataifa.

“Bodi ya pamba iendelee kutoa elimu kwa wakulima kuhusu kanuni 10 za kilimo cha pamba ili kuongeza ubora na tija katika sekta ndogo ya pamba,” amesema.

Wakulima wa pamba wamelipokea vizuri ongezeko hilo wakidai ni faraja kwao huku wakiahidi kuongeza uzalishaji katika msimu ujao.

“Natarajia kuvuna kilo 600 kutoka kwenye ekari tatu nilizolima msimu huu, ambazo zitaniingizia kiasi cha TZS 936,000 kwa bei elekezi iliyotangazwa na Serikali,”ameeleza mkulima.

Send this to a friend