Benki Kuu kuchunguza sarafu ya kughushi ya TZS 500 inayosambaa mitaani

0
50

Benki Kuu ya Tanzania (BOT) imeanza kuchunguza sakata la sintofahamu kuhusu sarafu ya shilingi 500 baada ya kuonekana baadhi zikiwa na alama tofauti kwenye mzunguko wa biashara.

Uchunguzi uliofanywa na Mwanachi umeeleza kuwa, sarafu hizo zenye baadhi ya alama, zipo kwenye mzunguko na zinatumika kufanya manunuzi mbalimbali katika mazingira tofauti hususani jijini Dar es Salaam.

Akizungumza mmoja wa wafanyabiashara, George Migoba, mtoza ushuru katika moja ya huduma za choo jijini hapa, amedai karibu kila siku hupokea sarafu hizo katika harakati zake za biashara.

“Hii sarafu niliigundua miezi minne iliyopita, makondakta wengi wakija nazo hapa nawarudishia, au mteja anayetaka huduma, ukiitazama wamekosea kuikata halafu ni nyepesi, madini yake yako kama bati hivi,” amedai.

Aina ya watu wanaochelewa kufanikiwa

Baadhi ya alama zinazotajwa kuwa ni tofauti kwa mujibu wa mashuhuda wa sarafu hiyo, ni sarafu moja kuonekana inang’aa zaidi na nyingine imefifia, nyepesi na hata mlio wake ni tofauti ikiangushwa sakafuni.

Aidha, kwenye sura ya Rais wa kwanza wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Sheikh Abeid Aman Karume taswira ya nyati pia inaonekana tofauti na sarafu zingine.

Chanzo: Mwananchi.

Send this to a friend