Benki Kuu ya Argentina yapendekeza kuweka sura ya Messi kwenye noti ya 1000

0
19

Baada ya Lionel Messi kushinda Kombe la Dunia la FIFA huko Qatar, Benki Kuu ya Argentina inafikiria kuweka sura wa mchezaji huyo mashuhuri wa PSG katika noti ya 1000 kutokana na heshima aliyoipa taifa hilo.

Kulingana na gazeti la El Financiero, maofisa katika baraza la usimamizi wa fedha la nchi hiyo ya Amerika Kusini wanatafuta chaguzi za kuashiria ushindi wa kihistoria wa Kombe la Dunia la taifa lao.

Gazeti hilo liliripoti kwamba chaguo hilo lilipendekezwa kwa mzaha hapo mwanzo na wanachama wa Benki Kuu ya Argentina, lakini baadhi ya viongozi walionekana kuwa na shauku na kulikubali wazo hilo.

Tanzania yavuna bilioni 12 kutokana na Kombe la Dunia

Aidha, inaelezwa kuwa viongozi hao walifanya mkutano kuhusu jambo hilo hata kabla ya fainali ya Kombe la Dunia.