Benki ya Dunia, na Tanzania zatofautiana viwango vya ukuaji wa uchumi

0
38

Uchumi wa Tanzania unatarajiwa kukua kwa asilimia 5.8 mwaka 2020 ikilinganishwa ukuaji wa asilimia 5.6 mwaka huu, ambapo ukuaji unatarajiwa kuongezeka hadi asilimi 6.1 mwaka 2021, ripoti ya Benki ya Dunia (WB) imeeleza.

Hata hivyo takwimu za serikali zilizotolewa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt Philip Mpango zinaonesha kuwa uchumi wa Tanzania kwa mwaka 2019 utakua kwa asilimia 7.1, kutoka asilimia 7.0 mwaka 2018. Dkt Mpango alisema kuwa katika nusu ya kwanza ya mwaka 2019 uchumi huo ulikua kwa asilimia 6.9 ikilinganishwa na asilimia 6.8 mwaka ulliopita.

Wakati serikali ikisema kuwa mwaka 2018 uchumi ulikuwa kwa asilimia 7.0, kwa upande wake Benki ya Dunia imesema uchumi wa Tanzania mwaka 2018 ulikua kwa asilimia 5.2.

Katika ripoti take WB imesema kuwa uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni nchini Tanzania umeshuka kwa theluthi moja na kufikia dola bilioni 1 kutoka dola bilioni 1.5 kati ya mwaka 2015 na 2018.

Mnamo mwezi Aprili mwaka huu Shirika la Fedha Duniani (IMF) katika ripoti yake iliyovuja lilisema kwamba sera zisizotabirika na zinazoingilia kati katika soko zinakandamiza ukuaji uchumi.

Send this to a friend