Benki ya Dunia yaipa Tanzania trilioni 1 kuboresha elimu

0
46

Benki ya Dunia (WB) imeipata Tanzania dola za Marekani milioni 500, sawa na TZS trilioni 1.2 kwa ajili ya kuboresha elimu ya awali na msingi Tanzania Bara.

Fedha hizo ambazo zitawanufaisha zaidi ya wanafunzi milioni 12 katika ngazi mbili za elimu, zitawezesha pia elimu kuwa jumuishi zaidi, salama, WB imeeleza katika taarifa yake.

Aidha, lengo likiwa ni kuimarisha ubora wa elimu, fedha hizo zitawezesha elimu inayotolewa kuwa rafiki kwa watoto, kuwajengea uwezo wa kimasomo walimu, kuwagusa wale anaoishi katika mazingira magumu na kuwafundisha ujuzi watoto hao.

Mkurugenzi wa WB Tanzania, Mara Warwick amesema kuwa Tanzania imepiga hatua kubwa sana kwa kupanua utoaji wa elimu na kupungua utofauti kati ya watoto wa kiume na wakike katika elimu ya awali na msingi.

Ameongeza kuwa kuwekeza kwenye elimu kwa watoto hasa wanaotoka kwenye mazingira magumu ni hatua muhimu katika vita dhidi ya umasikini.

Uandikisha wa watoto nchini Tanzania umeongezea kwa watoto milioni 2.5 tangu mwaka 2013 Tanzania Bara na sasa watoto milioni 12.3 wanasoma kwenye shule za awali na msingi.

Hata hivyo mfumo wa elimu bado unakabiliwa na changamoto mathalani maeneo ya vijiji ikiwa ni pamoja na watoto kuchelewa kuanza shule, mazingira yasiyo mazuri ya kujifunzia, msongamano wa wanafunzi, upungufu wa walimu na uelewa mdogo kwa baadhi ya walimu, WB imeeleza.

Send this to a friend